Thursday, 22 December 2016

ARSENAL YAMKOSA TENA JULIAN DRAXLER

Image result for julian draxler
Mshambuliaji Julian Draxler ambaye alikuwa akifukuziwa na klabu ya Arsenal yupo njiani kujiunga na mabingwa wa Ufaransa PSG. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ameshakubali mkataba wa miaka minne kukipiga PSG ingawa klabu yake ya Wolfsburg imesema kuwa mchezaji wake huyo hataondoka bila ya paundi milioni 34.
Julian Draxler ana miaka 23 na amekuwa akiwindwa na Arsenal kwenye kila dirisha la usajili linapowadia.

MAN U YAKARIBIA KUMVUTA VICTOR LINDELOF


Image result for victor lindelof
Moja kati ya habari kubwa katika soka zilizoripotiwa usiku wa December 21 ni kuhusiana na mpango wa Man United kukaribia kukamilisha usajili wa beki wa kati wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Club Benfica ya Ureno Victor Lindelof.
Mitandao kadhaa ikiwemo The Sun imeripoti kuwa Man United wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Victor Lindelof kwa dau la pound milioni 42, Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira alikwenda England kukamilisha dili hilo, lakini inaripotiwa kuwa Victor atajiunga na Man United January.
Kama habari hizo zitakuwa kweli na Victor Lindelof atasajiliwa kwa pound milioni 42, atakuwa amevunja rekodi ya usajili ya Rio Ferdinand alipojiunga na Man United 2002 akitokea Leeds United kwa dau la pound milioni 29.1 na kuwa beki ghali zaidi katika historia ya Man United, rekodi ambayo itakuwa inavunjwa baada ya miaka 14.