Tuesday 31 October 2017

TCU:TAARIFA MUHIMU KWA UMMA 2017/2018.

Image result for TCU TZ

TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inawatangazia waombaji walioomba kujiunga na masomo ya shahada za kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18.
Hata hivyo Tume imebaini idadi kubwa ya waombaji wamerudia kuomba udahili, wamejithibitisha zaidi ya chuo kimoja au wamechaguliwa katika vyuo zaidi ya kimoja. Waombaji hao wamegawanyika katika makundi matatu:

a) Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja katika awamu zote tatu na bado hawajathibitisha KUONA BONYEZA HAPA

b) Waombaji waliothibitisha zaidi ya chuo kimoja KUONA BONYEZA HAPA

c) Waombaji waliokwisha kuthibitishwa vyuoni lakini wakaamua kurudia kuomba upya KUONA BONYEZA HAPA

Tume inaelekeza kwamba;
a) Waombaji walioorodheshwa hapa juu; wanatakiwa kuamua mara moja na kuripoti kwenye chuo kimoja na kufanya usajili katika chuo husika;

b) Tume inasisitiza kuwa waombaji hawa wanatakiwa kuwa wameripoti vyuoni na kusajiliwa kabla ya Tarehe 1 Novemba 2017.

Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
30 Oktoba 2017


Friday 6 October 2017

NEW: MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA DODOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

 Image result for UDOM
Chuo kikuu cha Dodoma kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2017/2018,majina haya ni wanafunzi ambao hawajachaguliwa chuo zaidi ya kimoja. KUONA MAJINA BONYEZA HAPA

NEW: MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DAR ES SALAAM(DUCE) 2017/2018

   Image result for duce tanzania                                                                 Image result for UDSM
    Chuo kikuu cha Dar es salaam kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho moja kwa moja yaani majina haya hayajachaguliwa zaidi ya chuo kimoja. Kulingana na wavuti ya chuo kikuu cha Dar es salaam wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wanatakiwa kuanza kuripoti chuo kuchukua admission letter pamoja na kuanza wiki ya utambulisho tarehe 28/10/2017.
MAJINA HAYA NI YA WANAFUNZI WA DUCE CAMPUS,KUYAONA BONYEZA HAPA

NEW: MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) 2017/2018

  Image result for UDSM
 Chuo kikuu cha Dar es salaam kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho moja kwa moja yaani majina haya hayajachaguliwa zaidi ya chuo kimoja. Kulingana na wavuti ya chuo kikuu cha Dar es salaam wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wanatakiwa kuanza kuripoti chuo kuchukua admission letter pamoja na kuanza wiki ya utambulisho tarehe 28/10/2017.
MAJINA HAYA NI YA WANAFUNZI WA MLIMANI CAMPUS,BONYEZA HAPA KUYAONA