TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inawatangazia waombaji walioomba kujiunga na masomo ya shahada za kwanza katika Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18.
Hata hivyo Tume imebaini idadi kubwa ya waombaji wamerudia kuomba udahili, wamejithibitisha zaidi ya chuo kimoja au wamechaguliwa katika vyuo zaidi ya kimoja. Waombaji hao wamegawanyika katika makundi matatu:
a) Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja katika awamu zote tatu na bado hawajathibitisha KUONA BONYEZA HAPA
b) Waombaji waliothibitisha zaidi ya chuo kimoja KUONA BONYEZA HAPA
c) Waombaji waliokwisha kuthibitishwa vyuoni lakini wakaamua kurudia kuomba upya KUONA BONYEZA HAPA
Tume inaelekeza kwamba;
a) Waombaji walioorodheshwa hapa juu; wanatakiwa kuamua mara moja na kuripoti kwenye chuo kimoja na kufanya usajili katika chuo husika;
b) Tume inasisitiza kuwa waombaji hawa wanatakiwa kuwa wameripoti vyuoni na kusajiliwa kabla ya Tarehe 1 Novemba 2017.
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
30 Oktoba 2017
No comments:
Post a Comment