Saturday, 7 April 2018

China kuchukua hatua ya kulipiza kisasi kwenye mvutano wa kibiashara kati yake na Marekani

Tokeo la picha la china vs usa national flag
Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, kama Marekani haitajali upinzani wa China na jumuiya ya kimataifa na kuendelea kufanya vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, China italipiza kisasi bila kujali hasara yoyote, itachukua hatua mpya za mfululizo kukabiliana na hali hiyo, na kulinda kithabiti maslahi ya taifa na wananchi wake.
Rais Donald Trump wa Marekani ametoa taarifa akisema, mwakilishi wa biashara wa Marekani anafikiria uwezekano wa kuongeza ushuru wa ziada wa dola bilioni 100 za kimarekani dhidi ya bidhaa China, huku akiongeza kuwa Marekani bado inataka kufanya mazungumzo.
Bw. Gao amesema, mvutano huo umesababishwa na upande mmoja wa Marekani, ambao uhalisi wake ni upande mmoja wa Marekani kupambana na pande mbalimbali za dunia na hatua ya kujilinda kibiashara ya Marekani inavuruga biashara huria duniani. China itaendelea kupanua mageuzi na ufunguaji wa mlango, kulinda mfumo wa biashara wa pande mbalimbali, kuhimiza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji duniani.

No comments:

Post a Comment