Friday, 13 April 2018

BARCELONA YAWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE

Tokeo la picha la joseph bartomeu barcelona
Rais wa Barcelona Josep Bartomeu ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu hiyo kutupwa nje katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Barcelona iliyokuwa ikipewa nafasi ya kusonga mbele, iliondolewa na AS Roma ya Italia baada ya kuchapwa mabao 3-0 ugenini.
Bartomeu amesema wamepokea kwa masikitiko matokeo hayo na kuwa Roma walikuwa katika kiwango bora uwanjani na walikuwa sahihi kusonga mbele.
Matokeo hayo yanafanya kibarua cha kocha Ernesto Valverde kinaweza kuota mbawa.

No comments:

Post a Comment