Monday, 21 November 2016

KWANINI TUNAWEZA KUHISI MAUMIVU YA WENGINE?







Image result for showing sympathy
Tunapoona marafiki zetu wamejeruhiwa, tunaweza kuhisi maumivu kama tumejeruhiwa sisi.
Wanasayansi wa neva wakitumia teknolojia ya kisasa ya kupima ubongo wamegundua kuwa maumivu mbalimbali yanaweza kuchochea baadhi ya sehemu ubongoni. Mtu aliyekatika mkono wake katika miaka mingi iliyopita bado anaweza kuhisi maumvi ya mkono uliokatika, mtu aliyekataliwa na mwingine anahisi maumivu moyoni, na tunapoona marafiki wamejeruhiwa pia tunahisi maumivu, mambo hayo yote yanasababishwa na shughuli za sehemu zinazohusiana na maumivu kwenye ubongo wetu.
Uwezo wa kuhisi maumivu ya wengine haumilikiwi na binadamu tu. Wanasayansi wamegundua wanyama wengi wakiwemo panya na sokwe wana uwezo huo, ambao unasaidia kuwahimiza kuwatunza watoto na wenzao kwa makini zaidi, na kuongeza uwezo wa kuishi. Lakini kuwasaidia wengine katika mazingira ya asili huenda kukaleta hasara ama hata hatari, hivyo kwa kawaida wanyama wanawasaidia wenzao tu. Binadamu pia wanafanya hivyo, tunaweza kuhisi zaidi maumivu ya wenzetu, lakini tunapoona wale wasio wenzetu wamejeruhiwa, hatuhisi maumivu.
Utafiti mpya pia unaonesha kuwa si kama tu panya wanaweza kuona na kusikia maumivu ya wengine, bali pia wanaweza kuyahisi kwa pua. Watafiti wamegundua kuwa panya mwenye maumivu anaweza kuwaambia wenzake maumivu yake kupitia harufu maalum, na wale wanaohisi harufu hiyo watakuwa rahisi zaidi kuhisi maumivu.

No comments:

Post a Comment