Sunday, 19 March 2017

UTAFITI: "SURA NA JINA VINA UHUSIANO",JE WAJUA HAYO?,PATA UNDANI WA UTAFITI HUO.

Image result for NAME AND FACE
Ni kweli sura ya mtu inahusiana na jina lake? Kikundi cha utafiti cha Kimataifa kimetoa ripoti kwenye gazeti la Tabia na Saikolojia ya Kijamii la Marekani ikisema ni kweli sura ya mtu inafanana na jinsi jina lake linavyoonesha.
Watafiti wamewataka mamia ya watu kuangalia picha za wageni, na kuchagua jina kwa kila mtu kutoka kwenye majina manne hadi matano. Asilimia 25 hadi 40 ya watu walichagua majina sahihi, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko kiasi cha kuchagua majina bila kuangalia picha ambacho ni asilimia 20 hadi 25.
Utafiti unaonesha kuwa tamaduni pia zinaathiri uwezo wa kuchagua majina sahihi, kwa mfano, wafaransa wana uwezo mkubwa zaidi wa kuhusisha majina ya kifaransa na sura za Wafaransa.
Baada ya kuifundisha kompyuta kuchagua majina kwa kutumia data za sura na majina ya watu laki moja, kompyuta inaweza kuchagua majina sahihi kwa asilimia 54 hadi 64 ya picha.
Watafiti wamesema utafiti unaonesha kwamba ni kweli majina yanaweza kuwaathiri watu, kwa mfano, kuwahimiza kubadilisha mtindo wa nywele zao. Watu wanapenda kufanya mambo kwa kufuata makadirio bila kujijua, na mwishowe kusababisha makadirio kuwa hali halisi.

No comments:

Post a Comment