Tuesday, 14 March 2017

ELIMU:TANGAZO KWA UMMA

NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WALIOHITIMU MWAKA 2014/2015 KURUDI NYUMA.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia wahitimu wote wa Stashahada na Shahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati wa mwaka 2014/ 15 na miaka ya nyuma, kuwa bado kuna nafasi za ajira, hivyo, wenye sifa watume maombi yao.
Wahitimu walioomba wakati Wizara ilipotangaza nafasi za ajira mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 wasiombe tena kwa kuwa mchakato wa ajira kwa wale wenye sifa unaendelea. Wahitimu walioajiriwa Serikalini wasiombe.
Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni hizi zifuatazo:-
  • Elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
  • Taaluma ya Ualimu (Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu -PGDE);
  • ‘Academic Trascript’ ya Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu-PGDE);
  • Cheti cha Kuzaliwa;
  • Wasifu (CV) unaoonesha majina matatu. Mwombaji ambaye vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria za kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti/nyaraka halisi – (Kidato cha 4, 6, Stashahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada) na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘File’ moja la ‘pdf’. File lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
  2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.
TANBIHI:
  1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 30 Machi, 2017.
  2. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
  3. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira.
  4. Wahitimu ambao waliomba awali mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 na nyaraka zao ziliwasilishwa kikamilifu na kupokelewa, majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz. Hao wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
  5. Tangazo hili haliwahusu wahitimu waliofaulu mtihani mwaka wa masomo 2015/16 baada ya kurudia masomo waliyoshindwa mwaka 2014/15.
  6. Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz
IMETOLEWA NA
Tarish M.K.
KATIBU MKUU
10/03/2017

No comments:

Post a Comment