Tuesday, 21 February 2017

UTAFITI:JE WAJUA UMRI WA MWEZI?

Image result for MWEZIImage result for MWEZIImage result for MWEZI
Wanasayansi wana maoni tofauti kuhusu umri wa mwezi. Utafiti mpya unaonesha kuwa mwezi ulizaliwa katika miaka bilioni 4.51 iliyopita. Umri huo ni mkubwa zaidi kuliko wanasayansi wengi walivyodhani.
Wanasayansi wengi wanasema katika miaka mingi iliyopita sayari yenye ukubwa wa Mars iligongana na dunia na vipande vya sayari hiyo na dunia vikagunda mwezi. Wametafiti umri wa mwezi kwa kuchambua sampuli za miamba ya mwezi zilizokusanywa na chombo cha safari ya anga ya juu cha Apollo. Lakini wamepata matokeo tofauti kutokana na njia tofauti ya uchambuzi, baadhi yao wanasema mwezi ulizaliwa miaka milioni 100 baada ya kuzaliwa kwa mfumo wa jua, na wengine wanasema ni miaka milioni 150 hadi milioni 200 baada ya kuzaliwa kwa mfumo wa jua.
Hivi karibuni watafiti kutoka tawi la Los Angeles la Chuo Kikuu cha California wametoa ripoti kwenye gazeti la Science Advances la Marekani ikisema wamechambua mawe madogomadogo ya Zircon yaliyopelekwa duniani na chombo cha Apollo mwaka 1971 kwa teknolojia ya kuthibitisha umri kwa mujibu wa kiasi cha uranium na risasi, na kugundua kuwa mwezi ulizaliwa miaka milioni 60 baada ya kuzaliwa kwa mfumo wa jua, na umri wa mwezi ni miaka bilioni 4.51. Watafiti hao wamesema matokeo hayo ni sahihi zaidi na yanaaminiwa.

1 comment: