Bayern Munich imeishishia kipigo Arsenal kwa magoli 5-1 katika mechi ya kwanza ya raundi ya mtoano ya Timu 16 ya UEFA Champions Ligi, iliyochezwa huko Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
Hadi Mapumziko Timu hizi zilikuwa Sare 1-1 baada ya Arjen Robben kutangulia kuifungia Bayern na Arsenal kusawazisha baada ya Alexis Sanchez kupiga Penati iliyookolewa na Kipa Neuer na kumrudia tena na kufunga.
Lakini Kipindi cha Pili, ndani ya Dakika 20, Bayern walifunga Bao 3 za harakaharaka kupitia Robert Lewandowski na Thiago Alcantara, na kuongoza 4-1.
Dakika ya 88, Thomas Muller akaipa Bayern bao lao la 5 na kupata ushindi mnono wa 5-1 kwa kuisambaratisha Timu ya Arsene Wenger.
Katika mechi nyingine, Mabingwa watetezi Real Madrid wameitandika Napoli kwa mabao 3-1 pia katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo iliyochezwa huko Santiago Bernabeu.
Napoli walitangulia kufunga kwa kombora la Lorenzo Insigne na Real kusawazisha kwa Bao la Karim Benzema. Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Real walikwenda mbele 2-1 baada ya kazi njema ya Cristiano Ronaldo na kumlisha Toni Kroos aliefunga. Bao la 3 la Real lilifungwa kwa kigongo cha Carlos Casemiro.
No comments:
Post a Comment