Thursday, 16 February 2017

UTAFITI:JE LUGHA NI KWA AJILI YA MWANADAMU PEKEE?


Jinsi binadamu walivyobuni lugha mbalimbali kabla ya miaka milioni 25 iliyopita ni suala kubwa ambalo bado halijapata ufumbuzi. Hivi karibuni wanasayansi wamesema huenda watapata jibu kutoka kwa sauti ya nyani aina ya baboon.
Wanasayansi kutoka vyuo vikuu sita kikiwemo Chuo Kikuu cha Grenoble Alpes wametafiti nyani 1,335 aina ya baboon, na kugundua kuwa baadhi ya sauti za baboon wa Guinea zinafanana na zile za binadamu.Image result for BOBOON
Kabla ya hapo, watafiti waliona ni lugha zilitokea baada ya nyani wanaofanana na binadamu wenye koo iliyoko chini zaidi kutokea duniani. Lakini utafiti mpya unaonesha kuwa hata baboon wa Guinea wamekuwa na uwezo wa kutoa sauti zinazofanana na binadamu. Watafiti pia wamegundua kuwa misuli ya ulimi wa baoon wa Guinea pia zinafana na zile za binadamu, ambazo zimewawezesha kutoa sauti hizo.
Watafiti wamesema binadamu wa kale hawakuwa na uwezo wa kuongea lugha ghafla, bali lugha zinatokana na sauti za nyani kabla ya miaka milioni 25 iliyopita. Watafiti pia wamesema baboon wanapotoa onyo au kuwachumbia jike, wanatoa sauti maalum zinazofanana na sauti za binadamu.
Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la Public Library of Science la Marekani.

No comments:

Post a Comment