Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 15 kwa Frikiki ya Zlatan Ibrahimovic iliyombabatiza Mchezaji wa St-Etienne Pajot na kutinga.
Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Zlatan Ibrahimovic alifunga Bao nyingine 2 katika Dakika za 75 baada ya kazi njema ya Marcus Rashford na jingine Penati ya Dakika ya 88 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Mvuto katika mechi hii ulikuwa ni kupambanishwa kwa mtu na Kaka yake Paul Pogba wa wa Man United na Kaka Mkubwa Florentin Pogba Beki wa St-Etienne ambae hakudumu Dakika 90 baada ya kuumia Dakika ya 79 na kubadilishwa huku Mdogo Mtu akikosa Bao kadhaa na kupiga Posti pia.
No comments:
Post a Comment