Sunday, 19 February 2017

CHURCHILL:VIUMBE WA SAYARI NYINGINE

Image result for winston churchill
Mtaalamu wa fizikia ya anga wa Marekani Bw. Mario Livio ametoa makala kwenye gazeti la Nature la Uingereza akielezea makala ya zamani inayohusu uwezekano wa kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine iliyoandikwa na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza hayati Winston Churchill.
Hayati Churchill aliandika makala hiyo yenye kurasa 11 mwaka 1939, na aliirekebisha miaka ya 50 karne iliyopita, lakini hajawahi kuitoa kwenye gazeti.
Katika miaka ya 80 karne iliyopita, mswada wa makala hiyo ulipelekwa katika jumba la makumbusho la Churchill nchini Marekani. Mwaka jana mkuu mpya wa jumba hilo aligundua makala hiyo, na kumwalika Bw. Livio kuithibitisha.
Kwenye makala hiyo yenye kichwa cha "Tuko peke yetu ulimwenguni?", hayati Churchill ameeleza fikra zake kuhusu viumbe vya sayari nyingine, amesema maji ni muhimu kwa viumbe, pia amesema joto la sayari linalofaa maisha ya viumbe linatakiwa kuwa juu ya kiwango cha kuganda na chini ya kiwango cha kuchemka.
Hayati Churchill pia alifikiri jinsi sayari inavyoweza kuwa na hewa, na uwezekano wa kuwepo kwa viumbe katika mfumo wa jua na nje ya mfumo huo.
Hayati Churchill ni waziri mkuu wa kwanza aliyeajiri washauri wa sayansi nchini Uingereza, kitendo kilichoonesha kuwa anatilia maanani sayansi.

No comments:

Post a Comment