Tuesday, 19 September 2017

Kwanini mbwa wanawapenda binadamu?

Image result for dogImage result for dog
Ili kufichua jinsi mbwa walivyobadilika na kuwa wanyama wa kufugwa na kupendwa na binadamu, wanasayansi wamethibitisha baadhi ya jeni zinazoweza kuwafanya mbwa kuwa watulivu.
Kabla ya hapo, baadhi ya wanasayansi waliona kuwa aina kadhaa za mbwa mwitu walibadilika kuwa mbwa wa sasa baada ya kufugwa na binadamu, lakini hawajui sababu ya kubadilika kwa tabia ya mbwa. Watalaamu wa urithi Bw. Bridgett von Holdt kutoka Chuo Kikuu cha Princeton na Bw. Monique Udell kutoka Chuo Kikuu cha Oregon wametafiti jeni za mbwa na kugundua chanzo cha utofauti kati ya tabia za mbwa na mbwa mwitu.
Wanasayansi wamefanya majaribio kwa mbwa 18 na mbwa mwitu 10. Kazi ya mbwa na mbwa mwitu ni kutafuta soseji iliyofichwa kwenye moja kati ya masanduku. Mbwa mwitu waliwashinda mbwa, hata binadamu walipokuwa karibu, mbwa mwitu waliweza kumakinika na kazi zao, lakini mbwa hawawezi, wanatumia muda mrefu zaidi kuwaangalia binadamu badala ya kutafuta soseji.
Wanasayansi wamepima jeni za mbwa na mbwa mwitu, na kugundua kuwa jeni za GTF2I na GTF2IRD1 za mbwa zimebadilika, ambazo zinawafanya wawe na hamu kubwa zaidi kwa binadamu.

Wednesday, 13 September 2017

MASWALI NA MAJIBU KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA 2017/18 ELIMU YA JUU.

MASWALI NA MAJIBU KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KWA 2017/18

1. Swali: Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa?
    
Jibu: Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewa kidogo kufunguka, mwombaji anashauriwa kutoka na kujaribu kuingia tena (refresh) katika mtandao ili aweze kundelea na hatua zinazofuata.  

2. Swali: Je ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi/mlezi

 Jibu: Vyeti vya kuzaliwa na kifo cha mzazi/wazazi lazima kihakikiwe/vihakikiwe na RITA kabla havijapakiwa (upload) na kuambatanishwa kwenye maombi ya mkopo kisha kutumwa HESLB.

3. Swali: Je kama nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambacho hakijahakikiwa na RITA, nifanyeje?

 Jibu: Uhakiki wa cheti cha kuzaliwa au kifo ni hitaji muhimu ili kukamilisha maombi ya mkopo. Ni lazima kuhakiki vyeti husika, kisha uvipakie (upload) kwenye OLAMS kwenye vidirisha vya kuambatanishia (attachments) na baadae vyeti vyote viliyohakikiwa vitumwe HESLB.

4. Swali: Kama sikuwahi kumfahamu mzazi wangu, nitajaza nini ?

Jibu: Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea au kusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au msimamizi zithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo nyaraka rasmi za kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.

 5. Swali: Je nikikosea applicant category natakiwa kufanya nini?

Jibu: Unatakiwa kusoma kwa umakini miongozo iliyotolewa na hatua muhimu ili usikosee katika kipengele chochote cha ujazaji na uwasilishaji wa ombi 2 lako. Ikiwa kuna taarifa iliyosahaulika au kurekebishwa baada ya kukamilisha na kuwasilisha maombi yako, unatakiwa kuandika barua ya kuomba kufanyiwa marekebisho, na kuituma HESLB kwa njia ya EMS.

 6. Swali: Nitafanyaje nikigundua kosa au upungufu wa taarifa baada ya kukamilisha, ku-print na kutuma maombi yangu?

Jibu: Unatakiwa kuandika barua ya kurekebisha/kusahihisha taarifa za kipengele husika, kisha uitumie HESLB kwa njia ya EMS.

 7. Swali: Je kama nimehitimu kidato cha sita au diploma mwaka 2017 nitaambatanisha nini?

Jibu: Kama umehitimu kidato cha sita mwaka 2017, unatakiwa kutaja index number ambayo itatumika kuhakiki matokeo kutoka mamlaka husika. Kwa mhitimu wa diploma, unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo (transcript).

 8. Swali: Kama nikilipa na nisipopata namba ya muamala ili nikamilishe maombi yangu, nifanyeje ?

Jibu: Ni lazima kuzingatia maelekezo na hatua muhimu ikiwa ni pamoja na zile za kulipia. Ikiwa utalazimika kulipia tena ili uweze kukamilisha maombi yako, unashauriwa kuandika barua HESLB yenye taarifa za muamala ulioshindikana, ili uweze kurejeshewa pesa yako baada ya kuhakikiwa kwa kushirikiana na watoa huduma wetu.

 9. Swali: Nitanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB, NMB, M-pesa, AirtelMoney, Tigo-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea?

Jibu: Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kuchagua na kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au sehemu uliyoko wakati ukifanya malipo.

 10. Swali: Kama mwaka jana au kabla nilikuwa na umri chini ya miaka 30, je mwaka huu naweza kuomba?

Jibu: Vigezo na sifa za kuomba na kupangiwa mikopo vya 2017/18 ndivyo vitakavyotumika kwa waombaji wenye sifa na uhitaji. Kila mwombaji anashauriwa kusoma mwongozo na maelekezo kwa umakini ili kujipima kama anakidhi sifa na vigezo husika kabla ya kuomba.

11. Swali: Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani, na ninatakiwa kulipia 25% kabla ya kuomba tena, je nitafikiriwa kwa vigezo vya zamani ?

Jibu: Waombaji wote watapimwa na kupangiwa mikopo kwa mujibu wa uhitaji wao na kwa kutumia mwongozo na vigezo vya mwaka huu wa 2017/18.

 12. Swali: Kama ninao wazazi wasiokuwa na uwezo, je niwasilishe uthibitisho wa aina gani ili kupata mkopo?

Jibu: Unatakiwa kusoma kwa umakini mwongozo wa mwaka 2017/18 ambao unaelekeza namna ya kuthibisha uhitaji wako wa mkopo. Muombaji ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na hali hiyo ithibitishwe na mamlaka husika. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwa uhalisia na ukweli wake.

 13. Swali: Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha masomo, natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu ?

Jibu: Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yako yatapimwa kwa mwongozo na vigezo vya mwaka 2017/18.

14. Swali: Nimelipa lakini HESLB haijanitumia ujumbe wa kuendelea na maombi, nifanyeje? 


Jibu: Unatakiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika. Kama utapata changamoto ya aina yoyote, unatakiwa kuwasiliana na Kitengo Cha Usaidizi na Watoa Huduma (HelpDesk) kwa namba ya simu +255 22 550 7910 au anuani pepe helpdesk@heslb.go.tz inayoonekana kwenye tovuti yetu kwa ajili ya ufafanuzi na msaada zaidi.

 15. Swali: Je nikiingiza namba yangu isiyokuwa ya NECTA, mfano ya nje ya nchi, nitawezaje kuendelea kuomba mkopo?

Jibu: Unatakiwa kuiandika namba-tambulishi (index number) iliyotumika (isiyokuwa ya NECTA), Majina yako kamili, Jinsia pamoja na namba ya simu kwa usahihi na ukamilifu, kisha tengeneza namba ya malipo (generate payment control number). Baada ya hapo mfumo utakupatia namba ya kidato cha nne tofauti na ile uliyojaza awali (Isiyo ya NECTA) kulingana na format yetu ya namba za kidato cha nne. Namba hii mpya itatokana na ile namba iliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA), 4 ukipata ugumu wowote usisite kuwasiliana na Kitengo cha Msaada (HelpDesk) kwa ufafanuzi zaidi.

 16. Swali: Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia ya simu inayoonyeshwa kwenye mtandao? 

 Jibu: Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi (HelpDesk), kwa simu +255 22 550 7910 au kwa barua pepe helpdesk@heslb.go.tz. Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto husika kwa njia ya barua pepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia kama itahitajika. Kumbuka kuandika mawasiliano yako ya simu itakayotumika kukupigia.

17. Swali: Kama niko mwaka wa pili au wa 3, naweza kuomba mkopo pia ?

Jibu: Muombaji ambaye tayari yuko chuoni, anaruhusiwa kuomba mkopo kama inavyofafanuliwa katika mwongozo wa mwaka huu. 




Friday, 1 September 2017

BODI YA MIKOPO(HESLB): MUDA WA KUTUMA MAOMBI WAONGEZWA HUKU 15,473 PEKEE NDIO WALIOKAMILISHA TARATIBU ZA KUTUMA MAOMBI

Image result for HESLB

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa siku saba kuanzia Septemba 4, 2017 hadi 11, mwaka huu ili waombaji wenye sifa wawasilishe maombi yao kabla ya kufungwa kwa dirisha la maombi.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mchakato wa uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/18 na kwamba HESLB imetenga jumla ya Sh bilioni 427 kwa mikopo yote. Kwa mujibu wa Badru, jumla ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2017/18, wanatarajiwa kupata mikopo ya elimu ya juu huku wanafunzi 93,292 wakiwa wanaendelea kupokea mikopo hiyo kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.
Badru alisema hadi kufikia juzi, jumla ya waombaji wa mikopo kwa njia ya mtandao walikuwa 49,282, kati yao waombaji 15,473 wakiwa wamekamilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kwa kufuata taratibu zote za uombaji zilizotolewa na Bodi. Alisema kwa takwimu za maombi hayo, wapo waombaji 33,809 ambao wapo katika hatua mbalimbali za kuambatanisha nyaraka zao za maombi na kuwataka wale ambao hawajakamilisha kuwasilisha maombi yao ya mikopo kama ilivyoelekezwa.
Alisema waombaji wa mkopo wanatakiwa kuambatanisha nyaraka zao kwenye mfumo wa mtandao wa maombi hayo (OLAMS) kukiwa na nyaraka zilizosainiwa na viongozi wa serikali za mitaa na makamishna a viapo au Hakimu na kuziweka katika mtandao huo. Badru aliwataka wale wanaotarajia kuomba, kutumia muda uliosalia kukamilisha maombi yao, na kuyawasilisha kwa mujibu wa maelekezo, huku wakitakiwa kusoma kwa makini maelekezo na kufuata hatua zote za kukamilisha maombi ya mikopo.
Alisema bodi ilifungua dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa mwezi mmoja kuanzia Agosti 6, 2017 ili kuwawezesha waombaji wenye sifa kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao (OLAMS).
Alisema mchakato wa kuomba na kupanga mikopo unaongozwa na sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo na miongozo inayoainisha sifa, utaratibu na hatua muhimu kwa waombaji wa mikopo. Badru alizitaja hatua muhimu kwa waombaji wa mikopo kuwa ni pamoja na kila muombaji kutakiwa kuwasilisha nyaraka za maombi ikiwemo fomu ya maombi iliyosainiwa na Kamishna wa viapo au wakili na Hakimu, nakala za vyeti vya taaluma zilizothibitishwa na kugongwa muhuri na kamishna wa viapo, wakili au Hakimu.