Ili kufichua jinsi mbwa walivyobadilika na kuwa wanyama wa kufugwa na kupendwa na binadamu, wanasayansi wamethibitisha baadhi ya jeni zinazoweza kuwafanya mbwa kuwa watulivu.
Kabla ya hapo, baadhi ya wanasayansi waliona kuwa aina kadhaa za mbwa mwitu walibadilika kuwa mbwa wa sasa baada ya kufugwa na binadamu, lakini hawajui sababu ya kubadilika kwa tabia ya mbwa. Watalaamu wa urithi Bw. Bridgett von Holdt kutoka Chuo Kikuu cha Princeton na Bw. Monique Udell kutoka Chuo Kikuu cha Oregon wametafiti jeni za mbwa na kugundua chanzo cha utofauti kati ya tabia za mbwa na mbwa mwitu.
Wanasayansi wamefanya majaribio kwa mbwa 18 na mbwa mwitu 10. Kazi ya mbwa na mbwa mwitu ni kutafuta soseji iliyofichwa kwenye moja kati ya masanduku. Mbwa mwitu waliwashinda mbwa, hata binadamu walipokuwa karibu, mbwa mwitu waliweza kumakinika na kazi zao, lakini mbwa hawawezi, wanatumia muda mrefu zaidi kuwaangalia binadamu badala ya kutafuta soseji.
Wanasayansi wamepima jeni za mbwa na mbwa mwitu, na kugundua kuwa jeni za GTF2I na GTF2IRD1 za mbwa zimebadilika, ambazo zinawafanya wawe na hamu kubwa zaidi kwa binadamu.
No comments:
Post a Comment