Zahra ambaye ni Afisa Mikopo
daraja la kwanza katika Kitengo cha Uchambuzi na Upangaji Mikopo,
alihitimu Shahada yake ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustino (SAUT) mwaka 2010 na kujiunga na HESLB mwaka 2012. Kwa sasa
yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha Shahada ya Umahiri katika
Uchumi katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Bi. Zahra Kitara
Mshindi huyo wa jumla amesema siri yake
kubwa imekuwa ni kujihoji kuhusu utendaji wake wa kazi wa siku hadi
siku akihakikisha anaondoa makosa na kuboresha kazi zake, “mimi
nimejiruhusu kuwa mtu wa kwanza kujipa changamoto mwenyewe, najua kuna
maeneo fulani labda jana sikufanya vizuri, nafikiria leo nifanyeje ili
niweze kuboresha na kufurahia kazi zangu”, alibainisha Zahra.
Awali akikabidhi vyeti na zawadi kwa Watumishi walioibuka bora kutoka Idara na Vitengo mbalimbali kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya HESLB, Dar es Salaam, Jumatano Mei 10, 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Bw. Abdul-Razaq Badru aliwapongeza walioibuka washindi lakini pia aliwapongeza wafanyakazi wote akisema juhudi za pamoja ndizo zimewawezesha walioibuka na kutunukiwa kufikia hatua hiyo.
Wengine walioshinda kutoka idara na vitengo mbalimbali ni Joyce Mgaya (Habari na Mawasiliano), Luhano Lupogo (Sheria), Saumu Mbwana (Utawala), Hidaya Karunde (Ukaguzi wa Ndani), Simon Manangu (TEHAMA), Sophia Saidan (Urejeshaji Mikopo), na Henry Kapinga (Manunuzi).
Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Utafiti (RAAWU) tawi la HESLB, kila mwaka wamekuwa na utaratibu wa kuwapongeza watumishi wanaojipambanua katika utendaji wao wa kazi ili kuongeza hamsa na tija miongoni mwao.

No comments:
Post a Comment