Polisi wa Japan wamechambua idadi ya watu waliofariki kwenye ajali za barabarani na kugundua kuwa mtazamo huo si sahihi.
Mwaka jana watu 3,904 walifariki kwenye ajali za barabarani nchini Japan, ambapo kati ya watu 1,338 walikuwa abiria. Miongoni mwa madereva na abiria wote walioathirika na ajali za barabarani, asilimia 0.36 ya abiria waliokaa kwenye viti vya nyuma, asilimia 0.32 ya madereva, na asilimia 0.27 ya abiria waliokaa kando ya madereva walifariki. Hivyo watu wanaokaa nyuma wako hatarini zaidi kuliko wale wanaokaa kando ya madereva wakati ajali zinapotokea.
Polisi wa japan wamesema, zamani ilikuwa hatari kukaa kwenye viti vya mbele, lakini magari yanayotengenezwa siku hizi yana mifuko ya hewa na mikanda ya viti, na madereva na abiria wanaokaa mbele wanalazimika kufunga mikanda, hivyo idadi ya vifo imepungua kwa kiasi kikubwa. Lakini abiria wengi wanaokaa nyuma bado hawafungi mikanda, na kuwafanya wawe hatarini wakati ajali zinapotokea.
No comments:
Post a Comment