Bw. Federica Bertocchini kutoka Italia aliona kwa bahati kuwa mfuga nyuki mmoja aliwakamata wadudu kadhaa wanaokula nta kwenye mzinga wa nyuki, na kuwaweka ndani ya mfuko wa plastiki. Lakini dakika chache tu wadudu hao walikula baadhi ya plastiki na kutoroka.
Baadaye mtafiti huyu aligundua kuwa wadudu hao wadogo wa nondo aina ya Pyralidae si kama tu wanakula plastiki, bali pia wanaimeng'enya na kuibadilisha kuwa kemikali ya Ethylene Glycol.
Kwa wastani kila mfuko wa plastiki unatumiwa na binadamu kwa nusu saa tu, lakini unahitaji mamia ya miaka kuoza katika mazingira ya kimaumbile, kwa sababu mfuko huo unazalishwa kwa kemikali ya Polyethylene, ambayo ina muundo imara na ni vigumu sana kuoza. Hivyo suala la kushughulikia takataka za plastiki limekuwa tatizo linalowasumbua wanasayansi kwa muda mrefu. Tofauti na Polyethylene, kemikali ya Ethylene Glycol inaweza kuoza udongoni au majini ndani ya wiki chache tu.
No comments:
Post a Comment