Monday, 26 September 2016

JE WAJUA NAMNA YA KUTUMIA FRIJI LAKO KWA USALAMA ZAIDI?


Hivi karibuni friji la familia moja huko Nan'an mkoani Fujian China lililipuka na kusababisha kifo cha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 6. Baadhi ya vyombo vya umeme vyenye ubora vikitumiwa kwa njia isiyo sahihi pia vinakuwa hatari. Zifuatazo ni njia zisizofaa kutumia friji.
1. Usiweke vyombo vingine vya umeme juu ya friji.
Baadhi ya watu wanaweka microwave na oveni juu ya friji, lakini vyombo hivi vya umeme vinatoa mawimbi mengi ya sumaku umeme hivyo vinavuruga mfumo wa kupooza na kipuri cha kudhibiti joto cha friji, na kusababisha friji kutumia umeme mwingi zaidi.
2. Usiweke vitu vinavyopasuka kwa urahisi kando ya tundu la kutoa hewa baridi ndani ya friji
Baadhi ya watu wanaweka mabakuli ya kigae kando ya tundu la kutoa hewa baridi ndani ya friji, lakini baridi kali huenda ikasababisha vioo kupasuka na kuwaumiza watu.
3. Usiweke vitu vinavyoweza kulipuka ndani ya friji
Kuweka pombe na soda ndani ya friji kwa muda mrefu ni hatari. Kileo kikilipuka ndani ya friji kitasababisha moto kubwa. Na soda ikiganda, na kuitoa nje ya friji, huenda italipuka mara moja.

No comments:

Post a Comment