Wednesday 7 September 2016

USWISI YAITANDIKA URENO

Uswisi imeichapa mabingwa wa Ulaya Ureno mabao 2-0 kwenye mechi yao ya ufunguzi wa kufuzu kombe la dunia kwenye kundi B.
Breel Embolo na Ahmed Mehmedi ndio walitia kimyani mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza
Ureno walikuwa uwanjani bila huduma za nyota Cristiano Ronaldo, ambaye amekuwa na jeraha tangu Juali wakati wa fainali za kombe la Euro.
Ufaransa nayo ambayo iko kwenye kundi A walitoka sare ya 0-0 na Belarus huku Sweden na Netherlands wakitoshana nguvu ya 1-1

No comments:

Post a Comment