Shirika la Afya Duniani WHO limetoa ripoti ikisema, kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 umri wa kuishi kwa binadamu umeongezeka kwa wastani wa miaka 5 na kufikia miak 71.4. Kasi hiyo ni ya haraka zaidi tangu miaka ya 60 karne iliyopita, lakini pengo kati ya nchi mbalimbali bado ni kubwa.
Ripoti hiyo imeorodhesha takwimu za nchi na sehemu 149 kote duniani, ambazo ni pamoja na kiwango cha kifo, maradhi na vigezo vya mfumo wa afya.
Ripoti hiyo imeonesha kuwa ongezeko kubwa la umri wa kuishi unaotarajiwa na binadamu linatokea barani Afrika, ambalo maisha ya waafrika yameongezeka kwa miaka 9.4 na kufikia miaka 60. Chanzo chake ni kuwa maisha ya watoto yameboreshwa, udhibiti wa malaria umeimarishwa na dawa za kukinga virusi vya UKIMWI zinatumiwa zaidi.
Mbali na hayo, ripoti hiyo pia imeonesha kuwa wanawake wa Japani wana maisha marefu zaidi duniani ambayo ni miaka 86.8 kwa wastani, huku wanaume wa Uswisi wakiwa na maisha marefu zaidi duniani ambayo nia miaka 81.3 kwa wastani.
No comments:
Post a Comment