Saturday 3 September 2016

UGUNDUZI:KEMIKALI INAYOWEZA KUTENGENEZA DHAHABU

Dhahabu ni moja ya malighafi zinazotumika kutengeneza mbao za elektroniki za simu za mkononi, televisheni na kompyuta. Watu wengi wanatumia kemikali zenye sumu ikiwemo Cyanide kutenga dhahabu hizi kutoka kwenye mbao hizi. Njia hii si kama tu inafanyika kwa ufanisi mdogo, bali pia inadhuru afya ya watu na kuchafua mazingira.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Edinburgh wamegundua kemikali maalum inayoweza kutenga dhahabu kutoka kwenye takataka za vyombo vya elektroniki kwa ufanisi mkubwa na njia isiyochafua mazingira.
Watafiti hao waliweka mbao za elektroniki kwenye maji yenye asidi ili kuyeyusha metali, halafu walitia mafuta yenye kemikali hiyo majini, na baadaye dhahabu inatengwa kutoka kwenye metali mbalimbali zilizoyeyuka.
Watafiti hao bado hawajadokeza jina la kemikali hiyo, lakini walisema inakadiriwa kuwa kemikali hii itawasaidia watu kutenga tani 300 za dhahabu kutoka kwenye takataka za vyombo vya elektroniki duniani kila mwaka.
Watafiti hao pia wamesema kemikali hii ikitumiwa viwandani, si kama tu itazalisha dhahabu nyingi kwa kutumia takataka na kukidhi mahitaji ya dhahabu sokoni, bali pia itasaidia kupunguza athari mbaya ya uchimbaji wa madini kwa mazingira.

No comments:

Post a Comment