Manchester United Jumamosi hii imerudisha furaha kwa mashabiki wake na
kuzidi kuwazamisha mabingwa watetezi wa Premier League baada ya kupata
ushindi wa mabao 4-1, Leicester Cty. United ambayo ilikuwa kwenye Uwanja
wa nyumbani, Old Trafford ilionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza
na kufanikiwa kuandika mabao yote manne huku nahodha wake, Rooney
akianzia benchi.
Kwa matokeo haya, United inaongeza alama tatu na hivyo kufikisha jumla
ya pointi 12 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo wamefanikiwa
kushinda michezo minne, imepoteza miwili na haijatoa sare. Mabao ya
United yalifungwa na: Smalling dakika ya 22; Mata (36), Rashford (39),
Pogba (42) huku lile la Leicester likiwekwa kimiani na Gray dakika ya
60.
No comments:
Post a Comment