atika miaka mingi iliyopita wanajimu hawakupata maoni ya pamoja
kuhusu jinsi mwezi ulivyozaliwa. Kimsingi waliwahi kutoa nadharia nne
kuhusu chanzo cha mwezi.
Nadharia ya kwanza ni kwamba mwezi uligawanyika kutoka katika dunia
yetu. Mwaka 1898, mnajimu George Howard Darwin alisema mwanzoni mwezi
ulikuwa ni sehemu moja ya dunia, lakini dunia ilizunguka kwa kasi kupita
kiasi na kusababisha mwezi kugawanyika katika dunia. Lakini sampuli za
miamba ya mwezi zilizopelekwa duniani na chombo cha anga ya juu
zinaonesha kuwa miamba ya mwezi ni tofauti kabisa na ile ya dunia, hivyo
nadharia hii si sahihi.Nadharia ya tatu inasema hewa na vumbi kwenye mfumo wa jua vilikusanyika pamoja na kuunda mwezi na dunia, hivyo vina chanzo cha pamoja. Lakini nadharia hii pia imekanushwa, kwa sababu sampuli za miamba ya mwezi zinaonesha kwamba mwezi una historia ndefu zaidi kuliko dunia.
Nadharia ya nne imekubaliwa na watu wengi zaidi, inasema wakati dunia ilipoanza kuundwa, iligongwa na kimondo. Vipande vya kimondo hiki vilikimbilia duniani, lakini kutokana na mvuto wa dunia, havikwenda mbali na kukusanyika pamoja na kuunda mwezi.
No comments:
Post a Comment