Saturday, 13 August 2016

AFYA:BAADA YA KUOGA KAGUA MWILI WAKO

Image result for BODY INSPECTION AT BATHROOM       

Baada ya kuoga, usiharakishe kutoka bafuni, kwanza kagua mwili wako mbele ya kioo, ukikagua kwa makini, pengine unaweza kugundua matatizo kadhaa ya afya.
1. Kwanza angalia nyusi zako, kama nyusi zako zinabadilika na kuwa nyembamba zaidi au kuwa fupi zaidi kila siku, basi uchukue tahadhari katika tezi lako;
2. Kagua mdomo na meno yako, kama ulimi wako umefifia, basi pengine damu imepungua mwilini, na ukiwa na madoa myeupe kwenye meno yako, usiwe na wasiwasi, hii ni kutokana na kutumia dawa za meno zenye floridi mara kwa mara
3. Halafu macho yako, ukiona macho yako yana madoa ya manjano, basi uwe na tahadhari na ugonjwa wa aini;
4. Na kama wewe ni mwanamke, ukigundua nywele zako zimepungua sana, lakini nywele katika sehemu nyingine kama tumbo na miguu zimeongezeka sana, basi utahadhari na ugonjwa wa ovari na bora uende hospitali kuangaliwa na daktari.
5. Kagua miguu yako, mishipa yako ya damu ikiwa na rangi ya zabibu na kujitokeza waziwazi na ukiona inauma, basi bora uende kwa daktari, kwani pengine umepata ugonjwa fulani wa mishipa ya damu.

No comments:

Post a Comment