Friday, 19 August 2016

SERIKALI KUJENGA KIWANDA KIPYA CHA MATAIRI

Image result for TYREImage result for TYRE
Serikali ya Tanzania imesema inakusudia kujenga kiwanda kipya cha matairi chenye teknolojia za kisasa ili kwenda sambamba na ushindani wa soko.
Akizungumza mjini Dar es salaam, katibu mkuu katika wizara ya viwanda, biashara na Uwekezaji wa Tanzania Bw Adelhelm Meru amesema serikali imeona haina haja ya kukifufua kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre ambacho teknolojia yake imepitwa na wakati.
Amesema sasa Tanzania inahitaji kuwa na kiwanda cha kisasa kinakachokwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ambacho kitazalisha bidhaa zenye ushindani sokoni. Ameongeza kuwa tayari ameunda kamati ya wataalamu wenye ujuzi wa kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda kipya. Desemba 2012 serikali ilisema inajiandaa kutumbukiza dola za Marekani milioni 20 (Sh bilioni 42) ili kukiwezesha kiwanda hicho kuanza tena kazi baada ya kusimama mwaka 2009 kutokana na kushindwa kuhimili ushindani mkali kutoka katika matairi yaliyokuwa yanaingizwa kutoka nje ambayo yalikuwa rahisi.

No comments:

Post a Comment