Friday, 12 August 2016
BRAZIL YAIBANJUA DENMARK NA KUTINGA ROBO FAINALI OLIMPIKI
Brazil wamefuzu robo fainali ya mashindano ya soka ya Olimpiki baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Denmark, usiku wa kuamkia jana.
Gabriel Barbosa alifunga goli la kwanza la Brazil kabla la mchezaji mwenzake Gabriel Jesus kufunga goli la pili la nchi hiyo. Baadaye, Luan alifunga goli la tatu la taifa hilo na goli la mwisho lilifungwa na Barbosa kuhakikisha kuwa Brazil wanasonga mbele kama washindi wa Kundi 'A'.
Wakati huo huo, Argentina na waliokuwa mabingwa wa Olimpiki ya London 2012, timu ya Mexico, wametupwa nje ya michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment