Tuesday, 9 August 2016
NJIA ZA KUJIKINGA KUKOROMA UNAPOLALA
Watu wengi wana tabia ya kukoroma wanapolala, lakini kukoroma siyo kuzuri sana kwani familia yako pengine ishindwe kupata usingizi vizuri kutokana na makelele ulnayoyatengeneza na kwa upande mwingine, kukoroma kunamaanisha kuwa pumzi zako haziko sawa, hata baadhi ya wakati kukoroma kunaweza kusababisha kukosa pumzi na kupelekea kifo. Kwa hivyo, tuangalie tips kadhaa zinazoweza kubadilisha hali hiyo:
Kwanza ni kuchagua mito laini na inayoweza kufanya shingo yako iwe vizuri, ambayo itasaidia kupumua;
Pili ni kutumia mashine ya (humidifier) ili hewa ndani ya chumba iwe ya unyevu na kuepuka koo yako kuwa kavu;
Tatu, kunywa asali kidogo kulainisha koo yako na usinywe pombe kwani inapandisha shinikizo lako la damu na kuwa juu na kubana koo lako pamoja na kuzuia pumzi.
Nne, kama tunavyosema kila siku, fanya mazoezi mara kwa mara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment