Meneja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger amesema hatma
yake katika klabu hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu
hiyo msimu huu yatakavyokuwa. Raia huyo wa Ufaransa mwenye miaka 66,
aliajiriwa mwezi Septemba 1996 kuiongoza klabu hiyo. Mkataba wake wa
sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.
Arsenal haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 2004
jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa
mashabiki wa klabu hiyo. Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhfa wa
kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua
nafasi ya Roy Hodgson.
No comments:
Post a Comment