Monday 15 August 2016

JEMIMA JELAGAT AILETEA HESHIMA KENYA RIO


Image result for JEMIMA  JELAGAT
Kenya imepata dhahabu ya kwanza kwenye mashindano ya olmpiki mjini Rio baada ya wwanariadha Jemima Jelagat Sumgong kutwaa ushindi wa mbio za marathon upande wa wanawake.
Jemima Jelagat alishinda katika mda wa saa 2 dakika 24 na sekunde nne mbele ya mzaliwa mwengine wa Kenya ambaye amechukua uraia wake Bharian Eunice Kirwa.
Bingwa wa dunia Mare Dibaba wa Ethiopia alikuwa wa tatu.
Kenya sasa ina mdeali moja ya dhahabu na mbili za fedha baada Vivian Cheruiyot kushinda fedha katika mbio za mita 10,000 upande wa wanawake naye Tanui akaishindia fedha katika mbio hizo upande wa wanaume.

No comments:

Post a Comment