Wednesday 17 August 2016

LIVERPOOL YAKATAA KUMUUZA BENTEKE KWENDA CRYSTAL PALACE

Image result for bentekeImage result for benteke
Klabu ya soka ya Liverpool imekataa ofa ya Paundi milioni 30 kumuachia mchezaji wake Christian Benteke kujiunga na Crystal Palace.
Kiasi cha Paundi milioni 23 sambamba na ongezeko la Paundi milioni 7 lilitolewa na Crystal Palace baada ya kukataliwa ka Paundi milioni 25.
Benteke mwenye miaka 25,amekosa namba mbele ya kocha Jurgen Klopp aliyeingia Klabuni hapo Oktoba mwaka jana huku akianza katika michezo nane tu la ligi kuu.
Alijiunga na Majogoo hao kwa ada ya Paundi milioni 32.5 mwezi Julai 2015 chini ya kocha wa zamani Brendan Rodgers huku akifunga magoli kumi.
Benteke ameonyesha matamanio ya kuondoka kama tu hayupo kwenye mipango ya Klopp.

No comments:

Post a Comment