Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania imetoa ufafanuzi juu ya wanafunzi wa SJUIT ambao walihamishiwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini,hatua hii imekuaja baada ya bodi kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi hao.
Bodi ya mikopo imesema ni wanafunzi 3,722 walitakiwa kuhamishiwa mikopo yao katika vyuo walivyohamishiwa lakini ni wanafunzi 3,374 pekee waliotimiza vigezo vya kuhamishiwa mikopo yao.Bodi ya mikopo imeongeza kuwa wanafunzi 348 pamoja na wale 335 wa SJUIT tawi la Arusha ambao walisimamishwa masomo kwa sababu mbalimbali mwaka 2014/2015,wamekosa sifa za kuendelea kupata mikopo.
Bodi ya mikopo imeongeza kuwa,kulikuwa na wanafunzi 13 ambao walikua wanasoma SJUIT na baadae kuhama katika vyuo vingine hapa nchini.
UFUATAO NI MCHANGANUO AMBAO BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU IMETOA
INSTITUTION NUMBER OF RELOCATED STUDENTS LOANS SUCCESSFULLY ALLOCATED STUDENTS REGISTERED TO OTHER INSTITUTIONS STUDENTS WHO WERE NOT LOANS BENEFICIARIES 2015/16
Marian University College 154 112 7 35
Mkwawa University College of Education 99 92 0 7
Mwenge Catholic University 718 700 0 18
Ruaha Catholic University 589 526 0 63
Sokoine University of Agriculture 1116 944 5 167
University of Dodoma 1046 1000 1 45
TOTAL 3722 3374 13 335
KUPATA ORODHA KAMILI YA MAJINA CLICK LINK IFUATAYO
No comments:
Post a Comment