Tuesday, 16 August 2016
MAN U WAMSAKA JOSE FONTE WA SOUTHAMPTON
Manchester United imeanza mazungumzo na Southampton kujadili uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati Jose Fonte.
Maneja wa Man United Jose Mourinho anasaka mchezaji mwenye uzoefu kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na hivyo basi huenda Fonte kutoka Ureno ndiye chaguo mwafaka.
Awali Man United walikuwa wamejadili uwezekano wa kumsajili Leonardo Bonucci kutoka Juventus lakini bado hawakufua dafu.
Fonte mwenye umri wa miaka 32 amekuwa na wakati mzuri uwanjani akiichezea Southampton na hasa kuisaidia timu hiyo kutwaa kombe la Euro 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment