Klabu ya Inter Milan imemteua aliyekuwa maneja wa Ajax Frank de Boer kuwa maneja wake mpya baada ya kumuachisha kazi Roberto Mancini.
Inter Milan ambayo ilinunuliwa na kampuni ya Suning ya China mwezi Juni imekuwa ikimlalamikia Mancini kwa uhamisho uisokuwa na mpango klabuni hapo.
Hata hivyo Milan hawajakuwa na siku za kufana uwanjani na walitandikwa mabao 6-1 na Tottenham ijumaa iliopita.
No comments:
Post a Comment