Wednesday, 17 August 2016

JOYCE NDALICHAKO ATOA SIKU SABA KWA VYUO VIKUU KUTEKELEZA HAYA



Image result for JOYCE NDALICHAKO CV
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ripoti juu ya uhakiki wa wanafuzi hewa,waziri JOYCE NDALICHAKO amesema kuwa zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu limekamilika kwa vyuo 31 kati ya vyuo 81 ambavyo vipo,amesema zoezi hili limefanyika kwa kututumia wafanyakazi wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na tume ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU.Waziri aliongeza kuwa zoezi hili la uhakiki limefanyika kwa awamu tatu ,katika awamu ya kwanza ilibainika wanafunzi2763 ambao walikuwa hajahakikiwa na baada ya awamu ya pili na ya tatu wanafunzi 2192 hawajahakikiwa mpaka sasa.waziri aliongeza kuwa mfano chuo kikuu cha Dar es salaam jumla ya wanafunzi  350 ambapo walitumia jumla ya tsh 703438635 hawakuhakikiwa,udom wanafunzi 364 ambapo walitumia jumla ya Tsh  460963550.
waziri ameongeza kuwa kwa wanafuzi ambao hawajahakikiwa mikopo yao imesitishwa kwani walipuuzia zoezi hili la uhakiki yaani jumla wa wanafunzi 2192.
na ndipo waziri alipotoa maagizo kwa vyuo vikuu vyote ambavyo viliidhinisha fedha za wanafunzi na baada ya zoezi la uhakiki kubainika hawako chuoni ametoa siku saba vyuo husika viwe vimerejesha fedha hizo kuanzia leo 17/08/2016 na hatua kali zitachukuliwa za kinidhamu na kisheria katika kufanikisha malipo ya wanafunzi ambao hawako chuoni na hii inawahusu wafanyakazi wa bodi ya mikopo na wafanyakazi katika vyuo vikuu husika.Lakini ameongeza kuwa katika uhakiki huo imeonekana kuna utofauti katika taarifa za matokeo zinazopelekwa bodi ya mikopo na taarifa halisi za wanafunzi hivyo waziri amesema utafanyika uhakiki mwingine kwani kuna madudu mengi.


No comments:

Post a Comment