Tuesday, 16 August 2016

MANJI AJIUZULU UENYEKITI YANGA

Image result for yusuph manji
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu wadhifa huo ndani ya klabu hiyo alioutumikia kwa takriban miezi miwili tangu aingie madarakani katika uchaguzi mkuu uliofanyika Juni 25 mwaka huu.
Mbali na kujiuzulu uenyekiti, Manji pia amesitisha mpango wake wa kutaka kuikodi timu kwa miaka 10 kama alivyowaahidi wanachama katika mkutano wa dharura, takriban wiki mbili zilizopita.
Duru zinaarifu kwamba Manji amefikia uamuzi huo kwa kile kinachodaiwa ni kuingiliwa mpango wake wa kutaka kukodi timu. Katika mkutano wake wa dharura na wanachama, Manji aliomba akodishiwe timu na nembo ya Yanga kwa miaka kumi na kwamba atatoa asilimia 25 ya faida kwa klabu na asilimia 75 atachukua yeye huku akisisitiza akipata hasara itakuwa yake.

No comments:

Post a Comment