Chelsea imeanza vyema harakati zake za ligi kuu kwa kuifunga West Ham
mabao 2-1 katika mechi iliochezewa uwanja wa Stamford Bridge,.
Eden Hazard ndiye aliyeanza kufungua bahati ya Chealsea baada ya
kufunga mapema kipindi cha pili huku naye James Collins akisawazisha
wakati mechi ikisalia na dakika 13.
Japo ilionekana kwamba mchezo utaishia kuwa sare ya 1-1 lakini
Diego Costa alizamisha ndoto ya West Ham alipopachika wavuni bao la pili
dakika ya 89.
No comments:
Post a Comment