Friday, 5 August 2016
KUTAZAMA RUNINGA KWA MASAA MENGI KUNAPELEKEA KIFO
Wanasayansi wa Japan wanasema kuwa utazamaji wa runinga kwa saa nyingi unaongeza hatari ya kufariki kutokana na tone la damu katika mapafu.
Watafiti walichunguza utazamaji wa runinga miongoni mwa watu 86,000 kati ya mwaka 1988 na 1990 na kuwafuatilia afya yao miaka 19 iliofuata.
Habari mbaya kwa watazamaji wa televisheni ni kwamba kwa kila saa mbili zaidi za utazamaji wa runinga kila siku, hatari ya kufariki kutokana na tatizo la mapafu inaongezeka kwa asilimia 40.
Utazamaji wa saa tano ama hata zaidi wa runinga kila siku huwafanya watu wengi kufariki ukilinganisha na wale wanaoangalia runinga chini ya saa 2.5 pekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment