Wednesday, 10 August 2016

JONAS JUNIAS AKAMATWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Image result for joNAS JUNIAS
Bondia wa Namibia Jonas Junias ambaye anashiriki michezo ya olimpiki huko Rio nchini Brazil, amekamatwa kwa tuhuma za kesi ya ubakaji.
Jonas Junias ambae alibeba bandera ya Namibia siku ya ufunguzi wa michezo hiyo amepelekwa katika moja ya megereza makubwa huko mjini Rio.
Polisi wa Brazil wanasema alimbusu mhudumu wa chumba kwa lazima katika kambi ya wanamichezo na alimuahidi kumpa pesa kama atakubali kufanya nae mapenzi.
Bondia wa Morocco Hassan Sada nae alikamatwa Ijumaa iliyopita lakini alikanusha tuhuma hizo lakini bado yupo chini ya usimamizi wa polisi.

No comments:

Post a Comment