Tuesday, 30 August 2016

VIUMBE;SAMAKI JIKE WANACHAGUA VIPI WAUME WAZURI?

Image result for female fish

Ni kawaida kwa wanyama jike kuchagua waume wazuri na kuzaa watoto wenye jeni nzuri. Lakini jambo hili si rahisi kwa samaki jike, kwani mayai yao yanaungana na shahawa majini, hivyo inaonekana hawawezi kuzuia mayai yasiungane na shahawa za madume wabaya. Kwa hiyo watafanyaje?
Mwanabiolojia Suzanne Alonzo kutoka Chuo Kikuu cha Yale na wenzake wametafiti samaki aina ya ocellated wrasse, na kugundua kuwa majike wana uwezo wa kuchagua kuzaa watoto wenye jeni nzuri.
Samaki dume wana sura na tabia tofauti, baadhi yao ni wakubwa wenye rangi ya kupendeza, wanajenga viota kwa mwani, na kuyalinda mayai kwa makini, lakini wengine ni wadogo na wavivu, hawawachumbii majike wala kuyalinda mayai. Bila shaka majike wote wanapenda kuzaa watoto na wale wanaofanya bidii. Lakini wale wavivu ni wajanja, wanakwenda kwenye viota vya wengine bila mwaliko. Jambo baya zaidi ni kwamba idadi ya mbegu za uzazi za kiume za wale wavivu ni milioni 4, lakini za wale wenye bidii ni milioni 1 tu.
Inaonekana kwamba madume wavivu watashinda, lakini matokeo ni tofauti. Theluthi mbili za mayai yataungana na mbegu za uzazi za kiume za madume wazuri. Majike wanafanya nini kutimiza hali hii?
Ukweli ni kwamba majike wanafunika mayai yao kwa majimaji ya ovari. Mbegu za uzazi za kiume za madume wazuri zina uwezo mkubwa wa kupita majimaji hayo na kufikia mayai kwa kasi zaidi, hivyo ingawa majike hawawezi kuwazuia madume wavuvi wasije, lakini bado wanaweza kuchagua baba wazuri kwa watoto wao.

No comments:

Post a Comment