Friday, 19 August 2016

SADIO MANE KUKOSA MCHEZO WA JUMAMOSI

Image result for sadio mane
Winga wa Liverpool Sadio Mane, yupo kwenye hati hati ya kukosa mchezo wa Jumamosi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, dhidi ya Burnley City, kutokana kusumbuliwa na maumivi ya misuli. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, raia wa Senegal, aliumia wakati wa mazoezi ya asubuhi siku ya Jumatano, katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo, Melwood. Taarifa zaidi zimedai winga huyo ameteguka maungio ya bega na yupo kwenye uchunguzi zaidi, na timu ya madaktari wa klabu. Akiwa amesajiliwa msimu huu wa majira ya joto, kutoka klabu ya Southampton, winga wa Liverpool Sadio Mane, amefanya makubwa kwenye safu ya ushambuliaji na kusaidia ufungaji na yeye mwenyewe kufunga pia.

No comments:

Post a Comment