Monday, 15 August 2016
MAN UNITED YAILAZA BOURNEMOUTH
Manchester United imeilaza Bournemouth kwa mabao 3-1 na hivyo kumfanya mkufunzi Jose Mourinho aanza vyema harakati zake za kushinda kombe la ligi ya Uingereza msimu huu.
Juan Mata,ambaye alitolewa baada ya kuanza katika kombe la Community Shield alianza kufunga baada ya mchezaji wa Bournemouth Simon Francis kufanya masikhara.
Wayne Rooney alifunga bao la pili kwa kichwa kabla ya Zlatan Ibrahimovic kupata bao lake la kwanza akiwa na Manchester United kupitia mkwaju wa yadi 25.
Adam Smith aliifungia timu hiyo ya nyumbani bao la kufutia machozi.
United walicheza mechi hiyo bila Paul Pogba,huku kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan akicheza kama mchezaji wa ziada baada ya Mata kuanzishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment