Kundi moja la vijana waliojawa na
ghadhabu na ambao walikuwa wamejihami na fimbo waliwavamia raia wa
Uchina wanaofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya Treni nchini
Kenya.
Wafanyikazi 14 wa China walijeruhiwa wakati wa shambulio
hilo katika eneo la Narok, takriban kikomita 200 kusini magharibi mwa
mji wa Nairobi.
Washambuliaji hao walidaiwa kulalamikia kampuni ya
kujenga barabara na madaraja ya China kwa kutowapatia ajira za ujenzi
wa reli hiyo.
Makumi ya maafisa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo huku mamlaka ikifanya mikutano ya dharura kwa lengo la kutuliza hali.
Kuna
Takriban raia 4000 wa China wanaofanya kazi nchini Kenya hususan katika
viwanda vya ujenzi pamoja na biashara za kuuza vifaa vya
kielektroniki.
No comments:
Post a Comment