Friday 12 August 2016

JUAN MATA YAMTUMBUKIA NYONGO MAN UNITED

Image result for JUAN MATA
Kitendo cha kocha mpya wa Man United JoseMourinho kumuingiza Juan Mata dakika ya 63 na kumtoa katika dakika za nyongeza katika mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Leicester City, kinaonekana kuchukuliwa kwa mtazamo tofauti na kutabiriwa kuwa maisha ya nyota huyo Old Trafford yatakuwa magumu.
Habari kutoka The Times inaripoti kuwa Juan Mata kwa sasa analazimisha klabu imuachie aondoke licha ya kuwa uongozi wa Man United hawana mpango wa kumuuza kwa sasa, lakini gazeti hilo pia linaripoti kuwa kocha wa Everton Ronald Koeman kaonesha dhamira ya kumuhitaji nyota huyo.
 Image result for JUAN MATA
 Suala la Juan Mata kuhusishwa kuondoka linaweza kutokea kutokana na Jose Mourinho kudaiwa kutomuhitaji, hali kama hiyo iliwahi kumkuta nyota huyo wakati yupo Chelsea na Jose Mourinho ila mwaka 2014 aliamua kuondoka klabu hiyo na kujiunga na Man United.

No comments:

Post a Comment