Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City.
Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande na Robert Snodgrass .
Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47.
Leicester City ndio mabingwa wa kwanza watetezi kushindwa mechi
ya kwanza ya msimu uliofuata kutwaa ubingwa enzi ya Ligi ya Premia.
No comments:
Post a Comment