Tuesday 30 August 2016

THIERRY HENRY APEWA KAZI UBELGIJI

Image result
Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema nyota wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry Henry, ambaye pia aling'aa sana akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake.
Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga.
Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.

No comments:

Post a Comment