Everton imemsajili mchezaji wa kimataifa Yannick Bolasie raia wa Dr
Congo anayechezea timu ya Crystal Palace kwa gharama ya paund milioni
25, kwa mkataba wa miaka 5.
Bolasie, mwenye umri wa miaka 27, alitumia misimu minne akiwa na timu
ya Palace baada ya kujiunga na timu ya Bristol City ya mjini London
mwaka 2012.
Aidha mshambuliaji huyo raia wa Congo DR amesema kuwa yeye kwenda
Everton siyo kwamba kazi imekwisha, anatakiwa kujituma kwa bidii zaidi.
Bolasie alicheza mechi 143 akiwa Palace na alifanikiwa kufunga magoli 13.
No comments:
Post a Comment