Saturday, 13 August 2016

KIONGOZI TANZANITEONE ATUHUMIWA KWA UBAGUZI

Image result for tanzaniteone
KAIMU Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TanzaniteOne, Manu Sharma, anatuhumiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa ni mbaguzi wa rangi na anayeminya maslahi yao bila sababu.

Mbali ya kuwa mbaguzi wa rangi, pia anatuhumiwa kuwa na tabia ya kunyanyasa wafanyakazi wa kiafrika na kuwalazimisha kula chakula ambacho hakimo miongoni mwa milo iliyoidhinishwa na uongozi, kuwacheleweshea mishahara na kuzuia kulipwa posho zao za ziada.
Akizungumzia tuhuma hizo kwa njia ya simu, Sharma mbali ya kukana tuhuma hizo, alisema zina lengo la kumchafua na kumchonganisha na wakurugenzi wake.
Alidai wafanyakazi wanapewa msukumo wa watu wenye wivu naye, hivyo hawezi kuzungumzia tuhuma ambazo si za kweli.
“Si kweli kuwa nanyanyasa wafanyakazi na si kweli kuwa mimi sina sifa za kuwa Mhasibu Mkuu. Hayo yote yanapikwa,” alisema Sharma na kukata simu.
Wakizungumza na gazeti hili jana kufafanua kuhusu tuhuma hizo, wafanyakazi wa mgodi huo walioomba kutotajwa majina gazetini walidai kuwa chakula wanachokula hakistahili kuliwa kwani ni kibovu na kinawekwa pilipili nyingi tofauti na vyakula walivyoidhinishiwa.
Mmoja wa wafanyakazi hao, alidai orodha ya mahitaji ya chakula inayowasilishwa kwa wakurugenzi ni tofauti na vitu vinavyonunuliwa. Alidai kuwa kwa sasa ni wafanyakazi wachache sana wanakula kantini ya TanzaniteOne iliyomo ndani ya mgodi huo, kutokana na aina ya chakula wanachopewa.
Tuhuma nyingine zinazomkabili Sharma ni wafanyakazi kutolipwa mishahara kwa wakati na kushindwa kufahamu fedha hizo ambazo hutolewa mapema anazifanyia kazi gani kwa muda wote wa zaidi ya wiki mbili zaidi.
Anatuhumiwa pia kugoma kuwalipa stahili wafanyakazi na kufikia hatua ya mali za TanzaniteOne kutaka kukamatwa na madalali wa mahakama.

Uongozi wa TanzaniteOne inayomilikiwa kwa ubia ya Shirika la Madini la Taifa (Stamico) na Kampuni ya Sky Associates Limited umesema kuwa unachunguza tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment