Wednesday, 17 August 2016
RAISI WA ZAMANI WA FIFA AFARIKI JOAO HAVELANGE
Aliyekuwa rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki akiwa na umri wa miaka 100.
Joao ambaye ni raia wa Brazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho hilo la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.
Alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA April 2013 kufuatia uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa,na kulazwa hospitalini mwaka uliofuata alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.
Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.
Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment