Tuesday, 16 August 2016
BENKI YA DUNIA KUSAIDIA KUENDELEZA JIJI LA DAR ES SALAAM
Benki ya Dunia imepanga kutumia dola milioni 195 za Kimarekani kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, DMDP.
Mradi huo umeanzishwa ili kuboresha mfumo wa mipango mji na kurahisisha upatikanaji wa huduma za umma, na unatarajiwa kutekelezwa katika manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni, ukilenga kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuzingatia zaidi kodi ya majengo, na ujenzi wa maeneo matano ya kutupa taka katika jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI George Simbachawene amesema, mradi huo utahusisha uboreshwaji wa barabara ndogo amabazo zinaungana na barabara za Vituo vya Mabasi ya Mwendo Kasi Dar es slaam DART, pamoja na ujenzi wa barabara za pembeni ili kuungana na barabara kubwa ndani ya wadi 14 Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment